
Polisi iliwakamata watu 25 kwa kukiuka amri hiyo huku huku ikitangaza kuwashikilia zaidi ya watu 500 tangu maandamano yalipoanza mwishoni mwa wiki. Awali meya wa mji huo Karen Bass, alisema aliweka amri hiyo ya kutotoka nje ili kudhibiti uporaji na uharibifu wa mali.
“Nilitaka watu wafahamu kwamba nimetangaza amri hiyo ya dharura ya kutotoka nje katika jiji letu hili la Los Angeles lengo kuu likiwa ni kuepusha uharibifu na kuzuia uporaji,” alisema Meya Bass.
Trump apeleka askari Los Angeles huku maandamano yakiendelea
Vitendo hivyo vimekuwa vikishuhudiwa katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Marekani na kuvuruga maandamano ambayo yalikuwa ya amani.
Maandamano hayo yaliyoanza siku ya Ijumaa na baadae kugeuka kuwa ya vurugu yalimlazimu rais wa taifa hilo Donald Trump kuchukua hatua ya kupeleka jeshi kuyadhibiti licha ya gavana wa jimbo la California kupinga uamuzi huo. Trump alisema hatokubali taifa kusambaratishwa