
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema marufuku ya kusafiri na kufungia mali za mawaziri hao, Waziri wa usalama wa taifa la Israel Itamar Ben-Gvir na waziri wa fedha Bezalel Smotrich, haviendelezi juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kutaka uamuzi huo kubatilishwa.
Rubio ameongeza kuwa Marekani inaendelea kusimama bega kwa bega na Israel huku akiwakumbusha washirika wake kutomsahau adui wa kweli katika vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.
Kulingana na Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy Mawaziri hao wa Israel waliowekewa vikwazo wamekuwa wakichochea vurugu dhidi ya wapalestina kwa miezi kadhaa na kuhimiza ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.
Uingereza imechukua uamuzi huo pamoja na Australia, Canada, New Zealand na Norway.