Manunuzi ya Ujerumani kwa Urusi yapungua kwa 95%

Haya yanafanyika wakati ambapo vikwazo ilivyowekewa Urusi kutokana na uvamizi wake wa Ukraine vikiwa vimesitisha biashara baina ya mataifa hayo mawili.

Kabla vita vya Ukraine vilivyoanzishwa na Urusi mnamo Februari 24, 2022na vikwazo 17 vilivyopitishwa na Umoja wa Ulaya, Ujerumani ilikuwa inanunua bidhaa za Urusi zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 37, hiyo ikiwa mwaka 2021.

Bidhaa ambazo Ujerumani inauza kwa Urusi zilipungua kwa asilimia 71.6 mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2021.

Awamu ya 17 ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa Urusi vilianza kutekelezwa mnamo mwezi Mei wakati ambapo mashambulizi ya Urusi kwa Ukraine yanaendelea bila kusita.

Mhudumu katika duka la kuuza dawa Ujerumani
Mhudumu katika duka la kuuza dawa UjerumaniPicha: Huang Yan/Xinhua/picture alliance

Umoja wa Ulaya tayari uko katika harakati za kuandaa mzunguko wa 18 wa vikwazo kwa Urusi.

Hadi nusu ya pili ya mwaka 2022, Urusi ilikuwa muuzaji muhimu wa nishati kwa Ujerumani ila kufikia mwaka 2024, miongoni mwa bidhaa kuu ilizokuwa inaiuzia Ujerumani zilijumuisha chuma, bidhaa za kemikali, chakula na chakula cha wanyama.

Ujerumani kwa upande wake iliiuzia Urusi bidhaa za madawa na kemikali pamoja na mashine mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *