
Takwimu hizo zinawakilisha ongezeko la asilimia 24 tangu mwezi Desemba mwaka 2024. Idadi hiyo iliyotolewa ya watu waliopoteza makaazi inasemekana kuwa kubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo.
Amy Pope Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, amesema wengi wa watu hao wamelazimika kuyahama makaazi yao mara kadhaa, na sasa wanaishi katika mazingira ambayo sio salama.
UN: Haiti huenda ikakabiliwa na ghasia zaidi
Haiti, taifa masikini katika eneo la karibian linaloyumba kisiasa, limekuwa likipambana na magenge ya wahalifu, yanayodaiwa kutekeleza mauaji, ubakaji uporaji na utekaji wa watu.
Mji Mkuu wa Port-au-Prince ndio ngome ya mapambano kati ya polisi na magenge hayo ya wahalifu, lakini vurugu hizi zimeendelea pia kushuhudiwa katika amaeneo mengine ya nchi.