Katika hatua ya kukabiliana na wimbi la ajali zinazoendelea kugharimu maisha ya Watanzania, Bunge limefanya marekebisho ya sheri…

Katika hatua ya kukabiliana na wimbi la ajali zinazoendelea kugharimu maisha ya Watanzania, Bunge limefanya marekebisho ya sheri…

Katika hatua ya kukabiliana na wimbi la ajali zinazoendelea kugharimu maisha ya Watanzania, Bunge limefanya marekebisho ya sheria kwa kuondoa jukumu la uratibu wa usalama wa usafiri wa ardhini kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) na kulikabidhi rasmi Kikosi cha Usalama Barabarani.

Marekebisho hayo yamepitishwa kupitia Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali uliowasilishwa na kupitishwa bungeni, na sasa unasubiri kusainiwa na Rais ili kuwa sheria kamili.

Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kupunguza ajali kwa kuimarisha usimamizi wa usalama barabarani kupitia vyombo vya usalama vya moja kwa moja.

#azamnewsupdates
✍️Ahmed Ally
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *