Maafisa sheria na urekebu wa Jeshi la Magereza wamehimizwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, haki na utu wakati wa kuwahudumia wafungwa na mahabusu.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awamu ya pili kwa maafisa hao, yanayolenga kuwaongezea ujuzi kuhusu huduma za msaada wa kisheria, mapokezi ya wafungwa magerezani na matumizi ya adhabu mbadala.
Mafunzo haya yanatarajiwa kusaidia katika kutekeleza kwa vitendo dhana ya haki jinai yenye kuzingatia utu na usawa kwa wote.
#azamnewsupdates
Mhariri| @official_jennifersumi