WFP yaonya raia wa Kusini mwa Khartoum wanakabiliwa na tishio la njaa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP limeonya kwamba Maeneo kadhaa kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum yamo hatarini kukumbwa na njaa, kutokana na kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Onyo hili la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP lilitolewa hapo jana siku ya jumanne, huku kukiwa na uhitaji mkubwa wa rasilimali nyingi, wakati huu WFP ikielezea kukumbwa na upungufu wa fedha za msaada wa chakula kwa mikoa iliyoharibiwa na vita.

Katika Mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva kwa njia ya video kutokea Port Sudan Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan, Laurent Bukera, amefahamisha kuwa kiwango cha njaa na ufukara vimeenea katika sehemu nyingi za nchi hiyo zilizokumbwa na vita.

Bukera amesema raia wengi wamekuwa wakiishi bila ya matumaini wala matarajio ya kupata chakula, hali ambayo pia inasababisha maafa zaidi.

Haya yanajiri wakati Umoja wa mataifa umeendelea kutoa wito kwa Jumuiya za kikanda kuchangia katika juhudi za upatikanaji wa amani kwenye nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *