Kifo cha kijana Mkenya aliyekuwa kizuizini: Uchunguzi wa maiti unakinzana na toleo la polisi

Albert Ojwang alikamatwa Jumamosi, Juni 7, kufuatia malalamishi kutoka kwa kamanda wa pili wa polisi. Alikufa usiku uliofuata akiwa kizuizini. Uchunguzi wa maiti uliofanyika siku ya Jumanne, Juni 10, unaonyesha kuwa alishambuliwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard

Kulingana na toleo la polisi kuhusu tukio, Albert Ojwang anadaiwa kugonga kichwa chake ukutani. Inadaiwa alipatikana akiwa amepoteza fahamu katika chumba alikokuwa anazuiliwa wakati wa ukaguzi. Kisha alipelekwa hospitali na kutangazwa kuwa amefariki baada ya kuwasili. Hata hivyo, toleo hili haliendani na matokeo ya uchunguzi wa maiti uliofanyika siku ya Jumanne.

“Sababu ya kifo iko wazi kabisa: aligandamizwa shingoni na kichwa chake kupigwa sehemu ngumu. Pia tumeona majeraha yaliyoenea mwilini mwake, jambo ambalo linaonyesha shambulio.” Haya ni majeraha yaliyosababishwa na kitu kutoka nje, Bernard Midia, mmoja wa madaktari watano waliofanya uchunguzi wa maiti, ameambia waandishi wa habari. Ikiwa kichwa kingegongwa kwenye ukuta, kungekuwa na ishara tofauti, kama vile kutokwa damu kwa mbele. Lakini damu tuliyobaini kichwani ilikuwa nyingi zaidi, usoni na pande ya nyuma ya kichwa. Unapojumlisha na majeraha mengine mwilini, kuna uwezekano mdogo kubaini kwamba haya yalikuwa majeraha ya kujidhuru.” Kulingana na daktari huyo, uchunguzi wa maiti pia ulionyesha dalili za kupingana na kile alichokuwa akifanyiwa.

Albert Ojwang, mwenye umri wa miaka ishirini, alikamatwa Jumamosi katika Kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa nchi, kwa chapisho kwenye X linalodaiwa kumtusi afisa wa polisi. Kisha alipelekwa Nairobi, ambako alilala kizuizini. Baba yake alifahamu kifo chake alipokuja kumtembelea siku iliyofuata.

Tangu matokeo hayo kutangazwa, hasira zimekuwa zikiongezeka kwenye mitandao ya kijamii. Wakenya wanadai haki na zaidi ya yote, kujiuzulu kwa kamanda wa pili wa polisi, Eliud Lagat, ambaye aliwasilisha malalamiko yaliyopelekea Albert Ojwang kukamatwa. Tayari polisi wametangaza kuwa wamewasimamisha kazi maafisa wote waliokuwepo wakati wa kuzuiliwa kwake ili kurahisisha uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *