Mashambulizi yaliyoratibiwa kusini-magharibi mwa Colombia yaua watatu

Maafisa wawili wa polisi na raia mmoja wameuawa siku ya Jumanne, Juni 10, kusini-magharibi mwa Colombia katika mfululizo wa milipuko iliyoratibiwa na mashambulizi ya kutumia silaha, polisi imesema. Mapigano ya mara kwa mara kati ya jeshi na wapinzani wa FARC hutokea katika Maeeo ya Cauca na Valle del Cauca.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jumla ya mashambulizi kumi na sita ya watu wenye silaha, mabomu yaliyotegwa katika magari, na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yamelenga vituo vya polisi na majengo ya manispaa huko Cali, jiji la tatu kwa ukubwa nchini Colombia, na manispaa kadhaa jirani, mkuu wa polisi Carlos Fernando Triana amekiambia kituo cha redio cha La FM. Idara za Cauca na Valle del Cauca ni eneo la mapigano kati ya jeshi na wapinzani wa kundi la zamani la Kikosi cha Wanajeshi la Mapinduzi la Colombia (FARC), ambalo lilitia saini makubaliano ya amani mnamo mwaka 2016.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi, wapiganaji hao wa msituni wanaadhimisha kumbukumbu ya kifo mwaka 2022 cha kamanda wa zamani aliyejulikana kwa jina la “Mayimbu.” Alitaja mashambulizi hayo kuwa ya “kijinga.”

Milipuko mbalimbali imerekodiwa katika maeno ya Valle del Cauca, ikiwa ni pamoja na Cali, mji mkuu wa mkoa, ambapo afisa wa polisi aliuawa, pamoja na Jamundi, Corinto, na Buenaventura, bandari kubwa zaidi ya Colombia kwenye Pasifiki. Mlipuko mwingine ulitokea El Bordo, iliyoko katika eneo la jirani la Cauca. Huko Corinto, mpiga picha wa shirika la habari la AFP ameandika uharibifu wa barabara na majengo yanayozunguka eneo hilo kufuatia mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari.

Mashambulizi yanayohusishwa na kiongozi wa upinzani wa FARC?

Katika idara hizi mbili na katika Amazon ya Colombia, wapinzani wa FARC kutoka Central General Staff (EMC), wakiongozwa na Ivan Mordisco, wanamiliki maeneo makubwa ya kilimo cha koka, kiungo kikuu katika kokeini. Kwa wiki kadhaa, uvumi umeenea kuhusu afya ya Ivan Mordisco, ambaye aliripotiwa kujeruhiwa wakati wa operesheni ya kijeshi, na uwezekano wake wa kukamatwa. Mashambulizi haya yaliyoratibiwa yanaweza kuhusishwa.

Rais wa Colombia Gustavo Petro, ambaye alifungua mazungumzo ya amani na makundi yote vya waasi na makundi ya wafanyabiashara haramu wanaoendesha harakati zao nchini humo, mzalishaji mkubwa zaidi wa kokeini duniani, analinganisha Ivan Mordisco na mfalme wa cocaine marehemu Pablo Escobar (1949-1993). Mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa na kundi lake yalivunjika mwezi Aprili 2024, wakati Mordisco alipoachana na mazungumzo hayo.

Mashambulizi haya yanajiri siku tatu baada ya jaribio la mauaji huko Bogota dhidi ya seneta wa mrengo wa kulia Miguel Uribe, 39, mgombea urais. Alipigwa risasi mbili kichwani na yuko katika hali mbaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *