Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Chiza Malando amesema amewaondoa kazini baadhi ya watumishi wa id…

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Chiza Malando amesema amewaondoa kazini baadhi ya watumishi wa id…

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Chiza Malando amesema amewaondoa kazini baadhi ya watumishi wa idara ya afya wanaotuhumiwa kupokea rushwa na kuwatolea maneno makali wagonjwa wanaofika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.

Chiza alitoa kauli hiyo baada ya kuitwa kutoa maelezo kufuatia malalamiko ya wananchi mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Stephen Wasira, ambaye yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku nne.

Leo, Juni 10, 2025 akiwa Tunduru na Namtumbo, Wasira amekutana na viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina, tawi hadi kata na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

#azamnewsupdates
✍️Mawazo Mwaijengo
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *