Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha, ofisi yake imefanikiwa kukusanya gawio la shilingi tril…

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha, ofisi yake imefanikiwa kukusanya gawio la shilingi tril…

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha, ofisi yake imefanikiwa kukusanya gawio la shilingi trilioni 1.028 kutoka kwenye mashirika ya umma na kampuni ambako serikali ina hisa.

Hili ni ongezeko la asilimia 68 ikilinganishwa na mwaka jana, linaloashiria ufanisi wa usimamizi wa rasilimali za umma pamoja na mafanikio ya kiutendaji katika taasisi hizo.

Ameeleza kuwa mafanikio haya yanatokana na maboresho ya mifumo ya ufuatiliaji na udhibiti wa mapato, pamoja na ushirikiano mzuri kati ya ofisi ya Msajili wa Hazina na mashirika husika.

#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *