Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema uwekezaji wa mitaji kwa mashirika ya umma umeongezeka na kufikia trilioni 86.29 mwaka 2024 kutoka trilioni 65 mwaka 2020, sawa na ongezeko la shilingi trilioni 21.1.
Mchechu ameeleza mafanikio hayo leo katika hafla ya makabidhiano ya gawio na michango kutoka taasisi na mashirika ya umma kwa Rais Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi