Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Fyandom ameitaka serikali kuwapatia makoti ya kujikinga na baridi kali askari polisi wanaofanya kazi katika Mkoa wa Mbeya.
Akijibu maombi hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amesema makoti ya kujikinga na baridi kali ni miongoni mwa sare ambazo askari wanaofanya kazi mkoani Mbeya hupewa.
Mikoa mingine inayopewa makoti ya kujikinga na baridi ni Iringa, Njombe, Songwe, Arusha, Rukwa, Manyara, Kilimanjaro, na Tanga.
#AzamTVUpdates
✍Jairo Mtitu
Mhariri | John Mbalamwezi