Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Eqdward Mpogolo amewataka madaktari bingwa wa Kliniki ya Matibabu ya Kibingwa ya Dkt. Samia walioanza utekelezaji wa kampeni hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo wilayani Ilala kuwafundisha madaktari wenzao wa wilaya hiyo na mkoa kwa ujumla ili wakati wa kukamilika kwa kliniki hiyo madaktari watakaosalia wawe na ujuzi wa kuendelea kuhudumia wagonjwa.
Mpogolo ameyasema hayo mapema leo alipokutana na madaktari hao kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya jijini Dar es Salaam ambapo pia amewahimiza wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwenye kliniki hiyo maalum itakayodumu kwa siku sita.
Imeandaliwa na @moseskwindi