Licha ya jukumu lao kubwa la kulinda usalama wa watu na mali, baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi wameonyesha kuwa wana vipaji vya ziada ikiwemo muziki na burudani.
Mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa polisi baadhi ya askari walitumbuiza kwa sebene kali na kuonyesha upande wao mwingine wa burudani uliowafurahisha wengi.
Ni ushahidi kuwa nyuma ya sare, kuna vipaji vya kuvutia vinavyoweza kuhamasisha jamii kwa njia tofauti.
#azamnewsupdates
Mhariri| @official_jennifersumi