Sudani: Mapigano yahamia majimbo ya Kordofan

Tangu siku ya Alhamisi, Juni 5, mapigano yamekuwa yakiripotiwa katika majimbo ya Kordofan na kutishia kusambaa hadi katika jimbo jirani la Darfur. Kupitia vita hii mpya, jeshi la Sudani linalenga maeneo kadhaa na vifaa vya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kati ya Kordofan na Darfur. Pia linalenga, kwa mujibu wa taarifa rasmi, kupoteza rasilimali zao za silaha ili kuvidhoofisha huko Darfur.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, mapigano makali zaidi yametokea huko Kordofan Kusini, ambapo Vikosi vya Msaada wa Haraka vinapigana bega kwa bega na kundi la Ukombozi wa Watu wa Sudan (SPLM-N).

Kufuatia mashambulizi yake ya anga, jeshi limefanikiwa kudhibiti miji ya Dibebad na Hamadi. Lengo ni kupunguza mashambulizi katika miji ya Dalanj na Kadugli, ambayo imezingirwa na RSF. Jeshi pia limechukua udhibiti wa Kauda, ​​likitishia moja kwa moja makao makuu ya el-Helou huko Um Dehilib. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, ngome yake huko Babanusah inaendelea kushikiliwa baada ya mashambulizi makali ya RSF.

Ndege za jeshi ziliingilia kati mara kadhaa, zikilenga misafara ya ya magari ya vikosi vya wanamgambo hawa waliokuwa wamekuja kusaidi RSF ili kupunguza mashambulizi yao ya ardhini. Maghala yao ya silaha na risasi pia yamelengwa.

Siku ya Jumatatu, mji wa el-Obeid huko Kordofan Kaskazini ulikumbwa na shambulio la pili mfululizo la ndege zisizo na rubani za RSF. Raia watano waliuawa katika soko la mji huo wakati wa mashambulizi haya. Miji mingine kama vile El-Rahad na Dabanga pia ilikumbwa na mashambulizi haya. Kutoka kwa ngome zao kusini na kaskazini mwa jimbo hili, RSF inalenga kwa mashambulizi miji kadhaa kwa silaha nzito.

Katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Kordofan Magharibi, linalopakana na Sudan Kusini, mapigano makali yalitokea, haswa katika miji miwili ya Khouy na En Nahud. RSF ilishambulia vijiji kadhaa, kupora nyumba, kukata mawasiliano, na kuwalazimisha wakaazi kukimbia. Ndege za jeshi zililenga maghala na vituo vya silaha vya RSF katika mji wa Abu Zabad.

Barabara ya kimkakati

Barabara inayounganisha Khartoum na Kordofan, inayochukuliwa kuwa njia ya kimkakati kwa RSF, pia inalengwa na jeshi, kwani linataka kuidhibiti kama utangulizi wa uingiliaji kati wake ujao huko Darfur. Barabara hii inajumuisha safu ya mbele ya ulinzi kwa wapiganaji wa RSF huko Darfur.

Hata hivyo, vikosi vya pamoja vya Darfur, vinavyopigana pamoja na jeshi, viliwakamata wapiganaji kadhaa wa Libya wa Marshal Khalifa Haftar nchini Sudani. Walikuwa wakisafirisha risasi kwa RSF, vikosi vya pamoja vilidai. Wapiganaji hawa ni kutoka Brigedi ya Sobol al-Salam, inayoendesha harakati zake kwenye mpaka wa kusini wa Libya. Wakitokea al-Kufra na kujaribu kufika Kordofan Kaskazini, msafara wao ulilengwa na jeshi la anga la Sudani. Brigedi ya Sobol al-Salam haikanushi hili, lakini inasema ni kutokana na kutokuelewana.

Tangu kuanza kwa vita, Marshal Haftar amekuwa akishutumiwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwa kusafirisha mafuta na risasi kwa RSF nchini Sudani. Kikosi hiki pia kinashiriki katika shughuli kadhaa za usafirishaji wa watu katika jangwa, ikiwa ni pamoja na biashara ya binadamu.

Mamia zaidi ya familia zimelazimika kuyahama makazi yao, na hivyo kuzidisha hali ya janga la kibinadamu nchini Sudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *