
Takriban watu 15 wamefariki Jumatatu katika ajali ya barabarani baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi kugongana na gari dogo kwenye barabara kuu kaskazini mwa Malaysia, karibu na mpaka na Thailand, idara ya huduma za dharura zimeripoti. Basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Sultan Idris, kaskazini mwa Kuala Lumpur, wakati lilipogongana na gari dogo saa 7:00 usiku Jumatatu (1:00 usiku saa za Ufaransa).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Watu 13 wamefariki papo hapo na wawili baadaye wamefariki hospitalini, huku wengine 31 wakijeruhiwa, mamlaka ya usimamizi wa majanga ya jimbo la Perak imesema katika taarifa.
“Basi lilipinduka na gari dogo likateleza kwenye mtaro,” chanzo hicho kimeongeza. “Baadhi ya waathiriwa wamefanikiwa kutoka wenyewe katika gari hilo, wengine wametolewa nje, huku wengine wakiwa bado wamenasa ndani ya basi,” imeongeza taarifa hiyo.
Idara ya huduma za dharura inasema kuwa vifaa vya hydraulic extrication vinahitajika kuokoa na kuwapata baadhi ya wahasiriwa kutoka kwa basi.
Malaysia ina kiwango cha juu cha ajali. Gazeti la The Star liliripoti mwezi Machi kwamba mtu mmoja alifariki kila baada ya saa mbili katika barabara za nchi hiyo.