Rais wa Mexico atoa wito kwa Washington kutowachukulia wahamiaji kama ‘wahalifu’

Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum ametoa wito kwa Marekani siku ya Jumapili, Juni 8, kutowachukulia wahamiaji kama wahalifu kufuatia shambulio huko Los Angeles ambapo, amebainisha, raia 35 wa Mexico walikamatwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Wamexico wanaoishi Marekani ni (…) wanaume na wanawake wenye busara na waaminifu ambao walikwenda Marekani kutafuta maisha bora na kuhudumia familia zao. Wao si wahalifu,” amesema wakati wa hotuba kwa taifa.

Ajira ya wahamiaji “pia inasaidia uchumi wa Marekani,” amesisitiza.

Wanajeshi wa Marekani walianza kuwasili Los Angeles siku ya Jumapili kwa agizo la Donald Trump, kufuatia siku mbili za maandamano wakati mwingine yenye vurugu dhidi ya sera yake ya uhamiaji. “Hatukubaliani na mbinu hii ya kushughulikia hali ya uhamiaji, ambayo haihusishi mashambulizi au ghasia,” ametangaza, akitoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za wahamiaji. Bi Sheinbaum amesema kuwa wanadiplomasia wa Mexico walikuwa wakiwasiliana na Wamexico 35 wanaozuiliwa nchini Marekani.

Siku ya Jumamosi iIkulu ya White House ilitangaza kutumwa kwa wanajeshi 2,000 wa kikosi cha walinzi wa taifa huko California huku kukiwa na ghasia za kupinga kufukuzwa kwa wahamiaji huko Los Angeles.

Makabiliano kati ya waandamanaji wanaopinga hatua ya kufukuzwa kwa umati iliyotolewa na Donald Trump yanaendelea huko Paramount, kitongoji cha watu wanaozungumza Kihispania cha Los Angeles, kulingana na picha zilizorushwa moja kwa moja na shirika la habari la AFP.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *