Wapalestina 10 wauawa Gaza wakitafuta msaada wa chakula

Shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema mashambulizi ya Israel siku ya Jumapili yamewaua takriban watu 10 wakiwemo wasichana wawili katika Ukanda huo.

Msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal, amesema miili ya watu waliouawa na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Nasser iliyo katika mji wa kusini wa Gaza, Rafah.

Watu hao walikuwa wakielekea katika kituo cha usambazaji wa misaada kinachoshukiwa kuwa na uhusiano na Israel na kinachoungwa mkono na Marekani, GHF, wakati vikosi vya Israel vilipowafyatulia risasi kwa madai kwamba walikatiza katika maeneo yasiyoruhisiwa ya vikosi vyao.

Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz, akisema kwamba ameliagiza jeshi kuuzuwia msafara wa misaada unaomjumuisha mwanaharakati wa mazingira wa Sweden, Greta Thunberg, kutokutia nanga kwenye Ukanda wa Gaza. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *