Trump atuma wanajeshi kuwadhibiti waandamanaji wahamiaji LA

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru wanajeshi wa kitengo maalum kutumwa mjini Los Angeles baada ya maandamano dhidi ya uvamizi wa wahamiaji.

Rais Trump amechukua uamuzi huo na kupuuza mamlaka ya gavana wa jimbo la California, Gavin Newsom, ambaye anaamini ni bora kutumia njia ya mazungumzo na sio nguvu dhidi ya waandamanaji.

Vurumai hilo limetokea baada ya siku mbili za makabiliano ambapo maafisa wa polisi walifyatua mabomu ya machozi kwenye umati wa watu waliokasirishwa na kukamatwa kwa makumi ya wahamiaji katika eneo hilo.

Tangu aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu, Trumpamekuwa akiendesha operesheni dhidi ya wale anaodai kuwa ni “wahamiaji wasio na vibali”, ambapo maelfu ya watu wamefukuzwa nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *