Jeshi la Urusi laingia mkoa wa Dnipropetrovsk

Ikiwa kauli ya Moscow itathibitishwa, basi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa jeshi la Urusi kuingia ndani ya mkoa wa Dnipropetrovsk ndani ya miaka mitatu ya uvamizi wake dhidi ya Ukraine. 

Hata hivyo, licha ya Urusi kusema imeitwaa mikoa mitano ya Ukraine, lakini hadi sasa haijatamka rasmi kwamba imeutwaa na mkoa huo.

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema vikosi vyake vya kitengo cha vifaru kilikuwa “kimefika kwenye mpaka wa magharibi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk na vinaendelea na operesheni kwenye mkoa wa Dnipropetrovsk.

Soma zaidi: Urusi yafanya mashambulizi makubwa Ukraine

Kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi kwenye mkoa mwengine wa Ukraine ni hatua yenye maana ya kimkakati na kiishara kwa vikosi vya Kiev baada ya miezi kadhaa ya kurejeshwa nyuma kwenye uwanja wa mapambano.

Hakukuwa na tamko la haraka kutoka Ukraine kuhusu taarifa hiyo ya Urusi.

Dnipropetrovsk mkoa muhimu kwa Ukraine

Katika mgogoro wa zaidi ya muongo mmoja kwanza baina ya Kiev na wanamgambo wanaoungwa mkono na Kremlin na kisha jeshi la Urusi, Ukraine haijawahi kamwe kulazimika kupigana ndani ya eneo hilo la hadi sasa.

Ukraine Urusi Dnipropetrovsk.
Athari za mashambulizi ya Urusi kwenye mkoa wa Dnipropetrovsk.Picha: State Emergency Service of Ukraine/Anadolu/picture alliance

Dnipropetrovsk ni kituo muhimu cha viwanda na uchimbaji madini kwa Ukraine na kusonga mbele kwa vikosi vya Urusi ndani zaidi ya mkoa huo kunaweza kuwa na athari kubwa sana kwa uchumi na jeshi la Ukraine, vyote viwili vikiwa kwenye hali ngumu kwa sasa.

Soma zaidi: Urusi yasema imezidungua droni 174 za Ukraine

Mkoa huo ulikisiwa kuwa na wakaazi milioni tatu kabla ya Urusi kuanza mashambulizi yake, ambapo milioni moja kati yao wanaishi kwenye mji wake mkuu, Dnipro.

Afisa mmoja wa jeshi la Ukraine aliliambia shirika la habari la AFP hivi karibuni kwamba Urusi inaweza kusonga mbele haraka kwenye mkoa huo ambao kwa kiasi kikubwa upo tambarare, ikichukuliwa kwamba kuna vikwazo vichache vya kimaumbile au vijiji ambavyo vingeliweza kutumika kama maeneo ya ulinzi kwa vikosi vya Kiev.

Mabadilishano wafungwa yasita

Hayo yanajiri wakati, matreni yaliyobeba miili ya wanajeshi wa Ukraine yameanza safari zake kutoka Urusi kuelekea mpaka wa Ukraine siku ya Jumapili. 

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Likimnukuu Luteni Jenerali Alexander Zorin, shirika la habari la Urusi (TASS) limesema kuna dalili kwamba ukabidhianaji wa miili hiyo huenda ukaahirishwa hadi wiki ijayo. 

Soma zaidi: Zelenskiy autaka ulimwengu uishinikze zaidi Urusi

Siku ya Jumamosi (Juni 7), Urusi ilisema kwamba Ukraine ilikuwa imeahirisha bila kutarajiwa mabadilishano ya wafungwa wa kivita na kuikubali miili ya wanajeshi waliouawa kwa muda usiojuilikana. 

Kiev ilisema madai ya Moscow si ya kweli isipokuwa Urusi inaitumia operesheni hiyo ya kubadilishana wafungwa na maiti kwa njia isiyo sahihi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *