Mali: Jeshi lajiondoa katika kambi kuu ya Boulkessi, iliyolengwa na mashambulizi ya wanajihadi

Jeshi la Mali limekamilisha zoezi la kujiondoa katika kambi kuu ya kijeshi katikati mwa Mali, kambi iliyoko katika mji wa Boulkessi. Kufikia Jumamosi, Juni 7, hakuna askari hata mmoja aliyekuwepo. Kambi hiyo ilikumbwa na mashambulizi mawili mabaya ya wanajihadi mwishoni mwa juma lililopita, moja likiwa limetekelezwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Hakuna mwanajeshi mmoja wa Mali aliyesalia katika kambi ya jeshi huko Boulkessi. Katika kambi hiyo ambayo sasa ni tupu, magari ya kijeshi yaliyotelekezwa bado yapo, pamoja na mahema machache na chakula, ambacho inawezekana kilikusudiwa kutolewa kwa wanajeshi ambao walikuwa wakishikia ngome hii.

Kambi kubwa katikati mwa Mali, kambi ya Boulkessi inachukuwa heka kadhaa. Ilishambuliwa na wanajihadi mara mbili ndani ya siku mbili. Shambulio la kwanza liligharimu maisha ya wanajeshi wengi. Washambuliaji hao waliokuwa na silaha nzito walifika kwa miguu, kwa pikipiki, na kwa lori.

Wakati wa shambulio la pili, kulingana na habari zetu, wanajihadi walitumia ndege zisizo na rubani. Baada ya kuondoka, msafara wa jeshi ulifika eneo hilo kwa lengo la kusaidia manusura wa mwisho kuondoka kambini.

Ili kuelezea kuondoka kwa haraka kwenye kami hii, chanzo cha kijeshi cha eneo hilo kinakataa neno “kutelekezwa kwa kambi” na kinapendelea kuzungumzia juu ya “kujiondoa kwa kimkakati.” Waangalizi, kwa upande wao, wanabaisha “kuongezeka kwa shinikizo” kutoka kwa wanajihadi wa kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM), linalohusishwa na Al Qaeda. JNIM imeongeza mashambulizi yake kaskazini, katikati na kusini mwa Mali katika wiki za hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *