
Wizara ya biashara imesema China inatilia maanani wasiwasi wa Ulaya na iko tayari kuanzisha njia ya kijani kwa maombi yanayokidhi vigezo.
Madini hayo adimu hutumika katika bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na betri za magari ya umeme. Miziezi ya hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa sekta mbalimbali kuhusu namna leseni za madini hayo zinavyotolewa na China.
Wiki hii, waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao, alikuwa na mashauriano na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya, Maros Sefcovic ambao kwa pamoja walijadili hatua za kurahisisha biashara baina ya pande hizo mbili.