Kundi la Wagner kuondoka lakini Urusi itaendelea kuwepo Mali

Hata hivyo Urusi kwa jumla itaendelea kuwasilishwa nchini Mali. Licha ya tangazo la mamluki wa Wagner, kikosi maalum cha Afrika, kinachodhibitiwa na Urusi kitabakia nchini Mali.

Kikosi hicho cha Urusi barani Afrika, (Africa Corps) kimeeleza kwenye mtandao wa Telegram kwamba kuondoka kwa mamluki wa Wagner hakutaleta mabadiliko yoyote kwa sababu kikosi hicho kitaendelea kuwepo nchini Mali.

Soma pia: Kundi la Wagner: Ni nini kilichobadilika?

Wizara ya ulinzi ya Mali bado haikutoa tamko mara ilipoombwa kuzungumzia juu ya hatua ya kundi la mamluki wa Wagner.

Katika wiki za hivi karibuni kumetokea msururu wa mashambulizi ambapo waasi nchini Mali walisema kuwa waliwauwa zaidi ya wanajeshi 100 na baadhi ya mamluki wa Wagner.

Mali | Wanajeshi wa kundi la Wagner kaskazini mwa Mali
Uwepo wa kundi la Wagner barani AfrikaPicha: French Army/AP/picture alliance

Kundi la waasi la Jama’a Nusrat ul-Islam wa al-Muslimin (JNIM), kanda ya Afrika magharibi kwenye eneo la Sahel, lilidai kuhusika na mashambulio hayo ikiwa ni pamoja na shambulio la bomu la siku ya Jumatano dhidi ya wanajeshi wa Mali na Urusi karibu na mji wa Bamako.

Ulf Laessing, mkuu wa programu ya Sahel katika Wakfu wa Konrad Adenauer wa Ujerumani, amesema katika mahojiano kwamba Urusi imekuwa ikitaka kulibadilisha kundi hilo la Wagner na nafasi yake ichukuliwe na kikosi chake maalum barani Afrika (Afrika Corps).

Mamluki hao wa Urusi wanalisaidia jeshi la Mali katika kupambana na waasi wenye itikadi kali na wakati huo huo wakiimarisha ushawishi wa Urusi katika masuala ya nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Soma pia: Kituo cha mafunzo ya kijeshi Mali chashambuliwa

Mamluki wa kundi la Wagner wanaofadhiliwa na Urusi, sasa wamesema wanaondoka Mali baada ya kuwapo nchini humo kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu ambapo wamekuwa wanapambana na waasi.

Kundi la Wagner limekuwapo nchini Mali tangu serikali ya kijeshi ya nchi hiyo ilipowatimua wanajeshi wa ambao pia waliokuwa wakipambana na waasi kwa muongo mmoja.

Je, tunajua nini kuhusu Kikosi cha Urusi kitengo cha Afrika?

Kikosi hicho kiliundwa kwa msaada wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi baada ya mwanzilishi wa kundi la mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, na kamanda Dmitry Utkin, kuongoza uasi wa kijeshi dhidi ya uongozi wa jeshi la Urusi na baadae kuondoka kwenda Belarus pamoja na mamluki wengine.

Soma pia: Jeshi la Mali lapata pigo katika eneo la kaskazini

Prigozhin, alikufa baadaye katika ajali ya ndege kaskazini mwa jiji la Moscow. Kwa mujibu wa tathmini ya shirika la habari la Reuters, takriban asilimia kati ya 70 na 80 ya kikosi cha Urusi barani Afrika (Africa Corps) kinatokana na mamluki wa zamani wa Wagner. Kwa mujibu wa tathmini ya wataalamu wa Marekani, mamluki 2000 wamepelekwa kwenye kikosi hicho hicho nchini Mali.

Urusi | Yevgeny Prigozhin
Mwanzilishi wa kundi la Mamluki wa Wagner, marehemu Yevgeny PrigozhinPicha: Wagner Account/AA/picture alliance

Ulf Laessing, amesema kwa kikosi maalum cha Urusi barani Afrika hatua ya kuchukua mahala pa kundi la mamluki wa Wagner nchini Mali inamaanisha kuwa ushiriki wa kijeshi wa Urusi nchini Mali utaendelea, lakini huenda lengo likabadilika kwa kikosi hicho kuzingatia zaidi mafunzo na kutoa vifaa badala ya kutoa taswira ya kupigana na makundi ya waasi nchini Mali.

Chanzo: RTRE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *