
Tangu kutiwa saini mwezi Aprili mwaka jana kwa tamko la kanuni kati ya DRC na Rwanda-chini ya mwamvuli wa Marekani-Washington ina matumaini ya kuona makubaliano ya amani ya kweli mwishoni mwa mwezi Juni. Hata hivyo, ingawa mwezi huu umeanza, mazungumzo bado yanaendelea. Je, ni hatua gani imepigwa katika mchakato huu?
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu Aprili 25, tarehe ambayo lilitiwa saini tamko la kanuni huko Washington, mambo yamekuwa yakisonga mbele, ingawa kwa tahadhari. Rasimu ya kwanza ya makubaliano iliandaliwa kwa kuzingatia misingi ya mazungumzo yaliyofanyika Luanda, chini ya upatanishi wa Angola. Hoja mpya zimeongezwa, kutokana na matarajio ya Kinshasa na Kigali.
Leo, hati ya pili iliyofanyiwa kazi, toleo la marekebisho, linazunguka kati ya pande husika. Nakala hii inapaswa kutumika kama msingi wa majadiliano yajayo.
Kulingana na taarifa zetu, wajumbe wa masuala ya kiufundi kutoka Kongo na Rwanda wanatarajiwa mjini Washington wiki ijayo. Lengo: kutetea misimamo yao kabla ya kufanyika kwa mkutano rasmi kati ya mawaziri wa mambo ya nje.
Lakini katika ukanda, tahadhari bado zipo. Baada ya kushindwa huko nyuma, wanadiplomasia kadhaa wanasisitiza: hatupaswi kuharakisha mambo. Lazima “tufikie msingi wa mambo, tushauriane na washikadau wote, na kufikia makubaliano ambayo yatadumu.” Mwanadiplomasia mwingine wa Magharibi aliyeko Kinshasa anaongeza kuwa Washington lazima pia iunge mkono mienendo ya ndani na ya kikanda ambayo tayari inaendelea. Kwake, mchakato huu haupaswi kuzingatiwa kama mpango uliolazimishwa kutoka nje.