Wanajihadi wazidisha mashambulio katika nchi za Sahel

Wanajihadi wameendeleza mashambulio kwenye nchi za Sahel katika wiki za hivi karibuni katika nchi za Mali na miji kadhaa katika mataifa ya Burkina Faso na Niger.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashambulio hayo yameshuhudiwa kwenye nchi hizo tatu, zinazoongozwa na jeshi na kuendelea kutishia usalama wa mataifa jirani.

Siku kadhaa zilizopita, watu wenye silaha, waliwashambulia wanajeshi wa Mali na kusababisha maafa na majereha makubwa.

Ripoti za kiusalama, zinasema watu wanaojihusisha na Al-Qaeda na JNIM waliwauwa mamia ya wanajeshi wa Mali na Burkina Faso, huku kundi la Islamic State katika nchi za Sahel wakiendeleza mashambulio nchini Niger.

Watalaam wa masuala ya usalama, wanasema mashambulio hayo yanaongezeka kwa sababu ugaidi unabaidilika sana kutoka kiadilojia na sasa unageuka kuwa wa kikabila.

Mwezi Machi, viongozi wa kijihadi walitangaza  kuongeza mashambulio dhidi ya wanajeshi wa mataifa ya Sahel kwa kile walichokisema ni kuwalinda kabila la Fulani ambalo linaundwa na wakulima dhidi ya wanachosema ni mauaji ya kimbari.

Kuna hofu kubwa ya mashambulio haya kusambaa hadi katika nchi jirani za Togo na Benin, huku nchi hizo tatu za Niger, Mali na Burkina Faso zikiunda jumuiya yao, ya Sahel kipaumbele wakitoa kwenye mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *