
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M 23, wamewasilishiwa pendekezo la mkataba wa kusitisha vita, baada ya mashauriano waliyokuwa nayo nchini Qatar.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti zinasema wasuluhushi wa mazungumzo hayo ya Doha, wamewasilisha pendekezo hilo kwa kila upande na kutakiwa kushauriana miongoni mwao kabla ya kuurejesha. Hata hivyo, undani ya mkataba huu haujawekwa wazi.
Hii inakuja baada ya pande zote kuripotiwa kushiriki kwenye mazungumzo ya hivi punde na kujadili masuala yanayosababisha mzozo huo.
Aidha, ripoti zinasema, mazungumzo yanayokuja, yatakuwa muhimu sana kwa pande zote mbili, yanayolenga kutatua tofauti zinazosalia, katika majadiliano hayo yanayosimamiwa na Marekani pamoja na Umoja wa Afrika.
Wakati hayo yakijiri, Rwanda inayoshtumiwa kuwaunga mkono waasi wa M 23, mwezi Mei ilieleza kuwa mkataba kati yake na DRC kusaidia kumaliza mzozo huo, utasainiwa katikati ya mwezi huu wa Juni jijini Washington DC.
Mjumbe maalum wa Marekani barani Afrika, Massad Boulos naye pia siku kadhaa zilizopita, alisema, alikuwa amepokea rasimu ya mkataba wa amani kati ya Rwanda na DRC.