Zaidi ya watu 98 bado hawajulikani walipo juma moja baada ya mafuriko kuwaua watu 160 katika jiji cha Mokwa nchini Nigeria, idara ya majanga nchini humo imesema.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idara ya majanga nchini Nigeria imesema matumaini ya kuwapata manusura zaidi yamedidimia, na kuyataja mafuriko hayo kuwa mabaya zaidi kuwahi kuripotiwa nchini humo.
Juhudi za uokozi aidha zimelemazwa pakubwa na kuharibiwa na miundo mbinu, tahadhari ya kutokea kwa milipuko ya magonjwa pia ikitolewa, umoja wa mataifa nao ukisema umetuma kikosi chake kutoa huduma za dharura kwa maeneo yaliotahirika.
Raia katika maeneo yalioathirika hata hivyo wameendelea kulaumu serikali kwa kukosa kuweka mikakati ya kuzuia athari zinatokana na mafuriko.
Taifa la Nigeria hushuhudia mafuriko kipindi cha mvua ambazo huanza mwezi April hadi Oktoba, mwaka uliopita mwezi Septemba zaidi ya watu 30 walifariki kutokana na mafuriko na wengine mamilioni walipoteza makao, hali iliochangia hali ya binadamu kuwa mbaya zaidi.