Serikali ya Uganda, imekaribisha kwa mikono miwili uamuzi wa benki ya dunia ambayo imetangaza kuanza tena kutoa misaada kwa nchi hiyo baada ya kuisitisha mwaka 2023 kutokana na sheria tata kuhusu ushoga iliyopitishwa na bunge.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Benki ya Dunia inasema ina imani katika hatua mpya za kupunguza athari iliyopo ya ubaguzi na itairuhusu kusambaza ufadhili kwa njia ambayo haidhuru au kubagua watu wa LGBTQ.
Kwa mujibu wa taarifa ya AFP, benki hiyo inasema inashirikiana na serikali ya Uganda na wadau wengine nchini humo kuanzisha, kutekeleza na kufanyia majaribio hatua za kupinga ubaguzi.

Benki ya dunia ni mojawapo ya wafadhili wakubwa wa Uganda, ikifadhili miradi ya maendeleo, miradi ya miundo mbinu na kupambana na umaskini.
Mwaka 2023, Uganda ilipitisha sheria kali zaidi za kupinga mapenzi ya jinsi moja duniani ikimaanisha kwamba mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsi moja anaweza kuhukumiwa kifo.