Dunia yasherehekea mwanzo wa sikukuu ya Eid ul-Adha

Mahujaji siku ya Ijumaa wamefanya ibada kuu ya mwisho ya Hajj ambayo inahusisha “kumpiga mawe shetani”, wakati Waislamu wakiadhimisha mwanzo wa sikukuu ya Eid al-Adha.

Kuanzia alfajiri, mahujaji zaidi ya milioni 1.6 waliokuwa wakishiriki ibada ya Hija walirusha mawe saba kwenye kila kuta tatu za zege zinazoashiria shetani, katika bonde la Mina, nje kidogo ya mji mtakatifu wa Makka.

Ibada hiyo ni ukumbusho wa Nabii Ibrahimu aliyempiga mawe shetani katika sehemu tatu ambapo inaaminiwa kuwa Shetani alijaribu kumzuia Nabii Ibrahim asitii agizo la Mwenyezi Mungu la kumtoa mwanawe sadaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *