GHF yafunga vituo vyake vyote vya kusambaza misaada Gaza

Shirika la GHF linaloendesha utoaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza, ambalo linaungwa mkono na Marekani na Israel limesema hii leo Ijumaa kwamba limevifunga vituo vyake vyote vya kusambaza misaada hadi litakapotangaza tarehe mpya ya kufunguliwa tena vituo hivyo. Shirika hilo limewataka wakaazi kukaa mbali na vituo hivyo “kwa ajili ya usalama wao”.

Shughuli za shirika hilo zimesitishwa kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya Israel yanayosababisha vifo katika maeneo ya karibu na vituo vya ugawaji wa misaada. Shirika hilo linalolaumiwa vikali na mashirika ya misaada pamoja na Umoja wa Mataifa wanaolituhumu kutumiliwa na Israel, lilianza kusambaza misaada Gaza wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *