Qatar yawasilisha mswada wa amani kwa Kongo, waasi wa M23

Qatar yawasilisha mswada wa amani kwa Kongo, waasi wa M23

Chanzo kimoja kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa mazungumzo ya karibuni mjini Doha yalizingatia masuala ya msingi yaliyosababisha mgogoro wa mashariki ya Kongo.

Wapiganaji wa M23 ambao kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wanaungwa mkono na Rwanda wamesonga mbele kwa haraka mashariki mwa Kongo tangu mwezi wa Januari. Wameiteka miji muhimu na maeneo makubwa katika mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu.

Qatar imeshirikiana na Marekani katika juhudi za kuutatua mgogoro wa nchini Kongo. Chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa jina kwa sababu ya unyeti wa suala hilo kimeelezea awamu ijayo ya mazungumzo kuwa muhimu ambapo Kongo na M23 wanajiandaa kwa mazungumzo zaidiyatakayosimamiwa na WaQatari yakilenga kutatua tofauti zilizobaki.

Viongozi wa muungano wa AFC - M23
Kuna ripoti kuwa muungano wa AFC-M23 umewaondoa wajumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha bila kutoa taarifa rasmiPicha: Ernest Muhero/DW

Hata hivyo kumekuwa na ripoti kuwa muungano wa AFC-M23 umewaondoa wajumbe wake kwenye mazungumzo ya Doha bila kutoa taarifa rasmi. Hii imezusha uvumi kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo. Tovuti ya kibinafsi ya Habari Kivu imeripoti kuwa ujumbe huo ulirejea Goma, na mamambo yaliyojadiliwa hayajawekwa wazi.

Wachambuzi wamegawanyika kuhusu hilo, ambapo kuna wanaohisi kwamba makubaliano yanakaribia, huku wengine wakiuona kujiondoa huko kuwa ishara ya mkwamo.

Nayo tovuti ya habari ya Igihe nchini Rwanda inasema kujiondoa kimyakimya kwa muungano wa AFC-M23 kwenye mazungumzo ya Doha kunaashiria kushindwa kwa mazungumzo.

Majadiliano hayo yaliratibiwa na Marekani na Umoja wa Afrika. Rwanda ilisema mwezi Mei kuwa mkataba wa mwisho wa amani wa kuumaliza mzozo huo utasainiwa Katikati ya mwezi juu ya Juni mjini Washington.

Nani ananufaika na machafuko ya Kongo?

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Qatar ilifanikiwa kuandaa mkutano mwezi Machi kati ya Rais wa Kongo Felix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame. Viongozi hao wawili wakatoa wito wa kusitishwa mapigano baada ya mkutano huo.

Mwezi Aprili, Kongo na M23 walitoa taarifa wakiahidi kufanyia kazi amani, ingawa vyanzo katika kambi zote mbili vilionyesha subira juu ya kasi ya mazungumzo ya Doha. Kongo inasema Rwanda inaiunga mkono M23 kwa kuwapa askari na silaha. Rwanda inakanusha madai hayo, ikisema kuwa vikosi vyake vinajilinda dhidi ya jeshi la Kongo na wanamgambo wa Kihutu wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoua takriban watu milioni 1, wengi wao wakiwa Watutsi walio wachache.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *