
Mabao ya Uhispania yalifungwa na Nico Williams aliyefungua pazia la ushindi huo katika dakika ya 22, Mikel Merino, Lamine Yamal, Pedri na Lamine Yamal aliyehitimisha kwa bao la dakika ya 67.
Uhispania sasa itakutana na Ureno kwenye fainali zitakazochezwa Jumapili mjini Munich Ujerumani. Ureno ilitinga fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumatano.
Mechi hiyo ilitizamwa kwa upande mwingine kwa kuwashindanisha Yamal na Ousmane Dembele, wanaopigiwa upatu kushinda Tuzo ya Ballon d’Or.