
Siles amesema madai yaliyowasilishwa na serikali dhidi ya Morales ni ya ugaidi, kuuchochea umma kufanya uhalifu na kushambulia idara za usalama wa umma, miongoni mwa mengine.
Wafuasi wa Morales walianza kuweka vizuizi vya barabarani kuanzia La Paz kuliko na makao makuu ya serikali hadi katikati mwa Bolivia tangu siku ya Jumatatu na kulemaza shughuli.
Morales aliyekuwa rais kati ya mwaka 2006 hadi 2019 amezuiwa na mamlaka za uchaguzi na Mahakama ya Katiba kuwania awamu ya nne kwenye uchaguzi utakaofanyika Agosti 17.