Mtu mmoja ashukiwa kuambukizwa Ebola huko Jamhuri ya Czech

Mamlaka za Jamhuri ya Czech zilichukua hapo jana hatua kubwa za dharura na tahadhari baada ya kuripotiwa kisa cha mtu aliyeshukiwa kuambukizwa ugonjwa wa Ebola katika mji wa Tabori karibu kilometa 80 kusini mwa mji mkuu Prague.

Mtu huyo ambaye ni raia wa Marekani alirejea safarini hivi karibuni kutoka nchini Kongo, 
alihamishwa chini ya uangalizi mkubwa hadi katika kitengo maalum alikotengwa katika Hospitali ya Bulovka ya mjini Prague.

Hata hivyo, ripoti za vyombo vya ndani katika Jamhuri ya Czech hazijabainisha ikiwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 40 na anayeshukiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo hatari wa Ebola alitembelea nchi ipi kati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ama nchi jirani ya Kongo-Brazzaville. 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *