
Hiyo ni sehemu ya shinikizo la Marekani la kuutaka muungano huo wa kijeshi kuongeza gharama ya matumizi ya ulinzi. Malengo hayo yanaelekezwa kwa kila moja ya mataifa 32 kununua vifaa vya kipaumbele kama vile mifumo ya ulinzi wa anga, makombora ya masafa marefu, mizinga, ndege zisizo na rubani na “viwezeshaji vya kimkakati” kama vile kujaza mafuta ndege zikiwa angani, na usafirishaji wa zana nzito kwa kutumia ndege.
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutteamesema hayo yatafikiwa katika kikao cha mawaziri wa ulinzi leo mjini Brussels kabla ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi za NATO utakaofanyika The Hague mwishoni mwa mwezi huu. “Na uwekezaji huu wote unapaswa kufadhiliwa, na ndivyo tutafanya huko The Hague. Kwa hivyo hii ni njia ya hatua mbili, leo, ni malengo ya uwezo tunaotaka, ambayo tutawajulisha, kuhusu msingi wa majadiliano, kuwapa msingi wa mipango tuliyo nayo na ambayo inatokana na maamuzi tunayochukua leo na mawaziri wa ulinzi.”
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kuwa muungano sio kupeperushwa tu bendera za wanachama, bali kila mmoja kuchangia katika uwezekezaji.