‘Ishara mbaya’: Ujerumani inasitasita kutambua taifa la Palestina

Kutambuliwa kwa taifa la Palestina itakuwa “ishara mbaya,” amesema waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani siku ya Alhamisi, Juni 5, wakati nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Uingereza na Canada, zimesema zinazingatia kutambua taifala Palestina.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ujerumani inaendelea kudhihirisha uungaji mkono wake kwa Israeli na kuuzia suala la kutambuliwa kwa taifa la Palestina. Akiandamana na mwenzake wa Israeli, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul ameelezea kutambuliwa kwa taifa la Palestina kama “ishara mbaya.” Akiuchukulia msimamo wa Ujerumani kuhusu hali hiyo kuwa “wazi,” Wadephul hivyo amechukua mtazamo tofauti na Ufaransa, Uingereza, na Canada, ambazo zimesema zinazingatia kutambua taifa la Palestina.

Akijiweka sawa na msimamo wa Kansela Friedrich Merz, waziri huyo ameitaka Israeli kuruhusu misaada zaidi ya kibinadamu kwa Gaza, lakini pia akabainisha kuwa “Ujerumani itaendelea kuipa silaha Israeli,” akisisitiza kuwa taifa la Kiyahudi lazima lijilinde.

“Mchakato huu lazima ukamilishwe kwa njia ya mazungumzo kati ya Israeli na Palestina kabla ya kutambua taifa la Palestina, na tunaamini kwamba kutambua taifa la Palestina sasa kutatoa ishara mbaya,” amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Berlin, akiandamana na Gideon Saar.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje alithibitisha dhamira thabiti ya Berlin kwa Israeli, katika nchi ambayo bado inasumbuliwa na jukumu lake la mauaji ya Holocaust. Msimamo huu unaonyesha matatizo yanayokumba sera ya kigeni ya Ujerumani, kati ya uungaji mkono usio na masharti kwa Israeli na kuongezeka kwa shinikizo la kimataifa la kukomesha uhasama huko Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *