Xi Jinping azungumza kwa simu na Donald Trump katikati ya mvutanomkubwa wa kiibiashara

Rais wa China Xi Jinping amezungumza kwa simu na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, siku ya Alhamisi, Juni 5, kulingana na Xinhua, chombo cha habari cha serikali ya China, huku kukiwa na mvutano mkubwa wa kibiashara na kidiplomasia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ya simu yanakuja wakati mataifa hayo mawili yenye nguvu yanashutumiana kwa kuhatarisha mapatano ya kibiashara waliyoyajadili mwezi uliopita nchini Uswizi.

Viongozi hao wawili wamezungumza “kwa ombi” la Donald Trump, shirika la habari la Xinhua limeripoti, bila kutoa maelezo zaidi mara moja juu ya maudhui ya majadiliano.

Rais wa Marekani, ambaye ameiongoza Marekani katika zamu ya ulinzi mkali tangu arejee mamlakani mwezi Januari, alizua mzozo mpya na China siku ya Ijumaa.

Aliishutumu Beijing kwa kutoheshimu masharti ya mapatano ya kibiashara yaliyojadiliwa kati ya nchi hizo mbili mnamo Mei 12 huko Geneva.

Marekani na China zilifikia makubaliano ya kusitisha kwa muda vita vya biashara ambavyo vilisababisha kuongezwa kwa ushuru kwa bidhaa za Marekani hadi 125% na zile kutoka China hadi 145%.

Baada ya siku mbili za mikutano, Washington na Beijing zilikubali kupunguza kwa muda ushuru wao hadi 30% na 10% mtawalia, na kuahidi kuendelea na majadiliano kuelekea makubaliano ya biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *