
Algeria imewarudisha nchini Niger wahamiaji 16,000 kutoka mataifa mbalimbali, ambao waliwasili nchini humo tangu mwezi Aprili, wakitafuta njia ya kufika barani Ulaya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Idadi kubwa ya wahamiaji hao wamebainika kuwa raia wa Niger, lakini wengine ni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Magharibi na sasa wamerudishwa kwenye mji wa Assamaka unaopakana na Algeria.
Maafisa wanasema idadi hii ni kubwa, mara mbili ya wale waliofukuzwa kutoka Algeria mwaka uliopita.
Shirika lisilo la kiserikali nchini Algeria, Phone Sahara, linasema wahamiaji hao wanafukuzwa nchini Algeria wakiwa katika hali mbaya ya kibinadamu, na haki zao za msingi zinakiukwa.
Niger imekuwa ikipokea wahamiaji hao na mwezi Mei, Waziri wa Usalama Jenerali Mohamed Toumba, alionya kuwa hatua hiyo ya Algeria inahatarisha pia usalama wa nchi yake.
Aidha, Jenerali Toumba, amesema Niger kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wahamiaji IOM, litawarudisha wahamiaji zaidi ya Elfu nne, katika nchi zao walizotokea, kufikia mwezi Julai ili kuepusha hali mbaya ya kibinadamu.