
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anayezuru Paris, amemtaka mwenyeji wake, Rais Emmanuel Macron, kuunga mkono azma ya muda mrefu ya kuwa na mkataba wa ushrikiano wa kibiashara kati ta Umoja wa Ulaya na nchi za Amerika Kusini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi huyo wa Brazil amesema, hatoachia urais wa muungano wa kibishara wa nchi za Kusini mwa Amerika,hadi pale mazungumzo yatakapokamilika na umoja wa Ulaya na mkataba kutiwa saini.
Rais Da Silva ameongeza kuwa ushirikiano huo wa kibiashara utasaidia kupambana na hatua ya mataifa kama Marekani kutangaza nyongeza ya ushuru wa bidhaa kama alivyofanya Rais Donald Trump.
Mwezi Desemba mwaka uliopita, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, alitangaza majadiliano kuhusu mkataba huo wa ushirikiano ambao kila upande ungefaidika, lakini jitihada hizo zimekuwa zikipata pingamizi kutoka kwa Ufaransa na wanaharakati wa kilimo.
Ili mkataba huo upatikane na kuanza kutekelezwa ni lazima nchi 15 kati ya 27 za Umoja huo zitie saini za kuukubali.