Raia wa Burundi wameshiriki uchaguzi wa wabunge

Wananchi wa Burundi wamekuwa wakipiga kura kuwachagua wabunge, katika uchaguzi ambao chama tawala chake rais Evariste Ndayishimiye, cha CNDD-FDD kinatarajiwa kuibuka mshindi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura kuanzia Alfajiri, walijitokeza kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura kote nchini, kuwachagua wabunge.

Rais Ndayishimiye, aliungana na wapiga kura wengine katika mkoa wa Gitega, kupiga kura, akisifia namna wapiga kura walivyojitokeza kwa wingi kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi huu unafanyika wakati huu, Burundi ikiwa ikabiliwa na changamoto kubwa ya mafuta, baadhi ya wapiga kura tuliokutana nao, wamesema wanatumai, wabunge waliowapigia kura watasaidia kutatua changamoto hiyo.

Raia wa Burundi wanamatumaini kwamba wabunge wao wampya watawasaidia kutatua baadhi ya changamoto zao.
Raia wa Burundi wanamatumaini kwamba wabunge wao wampya watawasaidia kutatua baadhi ya changamoto zao. REUTERS – Evrard Ngendakumana

Wapiga kura wamewachagua wabunge 100,  na kwa mujibu wa Katiba, asilimia 60% lazima wawe  Wahutu walio wengi na asilimia 40% kutoka kwa Watutsi walio wachache, na takriban asilimia 30% ya wanawake.

Kwa uchaguzi wa manispaa, idadi ya manispaa imepunguzwa kutoka 119 hadi 42, lakini hakuna tena mgawo wa kikabila uliowekwa kwa vyama vya siasa, kama zamani.

Vyama vya upinzani kama CNL vinasema, uchaguzi huu unaegemea upande mmoja.

Jean Bosco Ndiyaragije, Ngozi, RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *