
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka saba hadi mwaka 2021, amefariki dunia akiwa hospitalini nchini Afrika Kusini, alikokuwa anapata matibabu.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kifo cha Lungu, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68, kimethibitishwa na familia yake na chama chake cha Patriotic Front.
Chama chake kimesema, rais huyo wa zamani, amepatwa na umauti, akiwa anapewa matibabu ya kibingwa kwenye kituo kimoja cha kiafya jijini Pretoria.
Binti yake, Tasila Lungu-Mwansa amesema, baba yake alihudumiwa vema, lakini hakueleza kwa kina kilichosababisha kifo chake.
Lungu, Mwanjeshi wa zamani, aliondoka madarakani mwaka 2021 baada ya rais wa sasa Hakainde Hichilema, na hadi kabla ya kifo chake, kiongozi huyo wa zamani alikuwa ametangaza kuwania tena rais mwaka 2026.