Ukraine na Iran katika ajenda ya mazungumzo mapya kati ya Trump na Putin

Donald Trump ametangaza siku ya Jumatano, Juni 4, kwamba amekuwa amezungumza na Vladimir Putin kuhusu Ukraine, ambapo rais wa Marekani haamini “amani ya haraka,” na kuhusu Iran, ambayo aliishutumu “kuvuta miguu” katika mazungumzo ya nyuklia. Kulingana na Donald Trump, rais wa Urusi anaweza kuwa na jukumu katika suala hili.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe kwenye mtandao wake wa Truth Social, Donald Trump amesema amekuwa na “mazungumzo mazuri na mwenzake wa Urusi, lakini sio mazungumzo ambayo yataleta amani ya haraka” huko Ukraine. Hii kauli tofauti na ile ya Mei 26, aliposema Vladimir Putin  “amechanganyikiwa.” Kulingana na bilionea huyo wa kihafidhina, wakati wa mkutano wa Juni 4, “rais Putin alisema, kwa uthabiti sana, kwamba atalazimika kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya hivi karibuni” ya Ukraine dhidi ya ndege za kivita za Urusi.

Rais wa Marekani amebainisha kuwa mazungumzo yao ya simu yamedumu “saa moja na dakika kumi na tano.” Kremlin, kwa upande wake, imeelezea mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao wawili kuwa “chanya” na “yenye tija,” na kuongeza kuwa wameamua “kuendelea katika mawasiliano ya mara kwa mara.”

Kuongezeka kwa operesheni za kijeshi kunaonekana kutanda nchini Ukraine, mbali na ahadi ya rais wa Marekani ya amani ya haraka, kutokana na kuingilia kati kwake. Katika mazungumzo ya simu na Papa Leo XIV, rais wa Urusi tayari aliilaumu Ukraine, akisema kwamba anataka kupata amani kwa njia za “kidiplomasia”, wakati, kulingana na yeye, Kyiv inatafuta “kuongezeka kwa uhasama” na “kufanya hujuma dhidi ya miundombinu ya kiraia kwenye ardhi ya Urusi.”

Mwishoni mwa wiki ya Mei 31-Juni 1, Ukraine ilitekeeza mashambulizi mabaya na makubwa kwa kutumia drone za kulipuka kwenye viwanja kadhaa vya ndege vya Urusi na kuharibu ndege nyingi za kijeshi. Kyiv pia ilidai kuhusika na shambulio kwenye bandari ya Kerch, bandari ya kishara, kwani inaunganisha Urusi na Crimea, eneo ambalo Moscow ilitwaa mnamo mwaka 2014.

Mazungumzo kati ya Kyiv na Moscow juu ya uitishwaji vita, ambayo Donald Trump alihimiza, yamekwama. Nchi hizo mbili zilikubali tu, wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Istanbul siku ya Jumatatu, kubadilishana wafungwa wote waliojeruhiwa au walio chini ya umri wa miaka 25, pamoja na miili ya askari 12,000 waliouawa (6,000 kutoka kila upande).

Donald Trump na Vladimir Putin pia wameijadili Iran. Rais Donald Trump hakujizuia wala hakuwa na subira, wakati Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ametangaza Jumatano kwamba pendekezo la Marekani la makubaliano ya nyuklia linakwenda kinyume na masilahi ya nchi yake, huku kukiwa na kutokubaliana juu ya kurutubisha madini ya uranium.

Rais wa Marekani ameishutumu Iran kwa “kuburuza miguu” katika mazungumzo hayo na kuongeza kuwa anataka “jibu la uhakika katika muda mfupi sana.” Pia ameripoti kwamba Vladimir Putin “amedokeza” kwamba anaweza pia “kushiriki” katika mazungumzo haya, ambayo yanafanyika hadi sasa kati ya Ira na Marekani.

“Nimemwambia rais Putin kwamba Iran haiwezi kupata silaha ya nyuklia, na ninaamini tunakubaliana kuhusu jambo hilo,” ameandika Donald Trump, akiongeza kuwa mwenzake wa Urusi, ambaye anadumisha uhusiano wa karibu na Tehran, “pengine anaweza kuwa na jukumu muhimu katika kufikia hitimisho la haraka.”

Kremlin siku ya Jumanne ilitetea “haki” ya Iran ya kuendeleza nguvu zake za nyuklia za kiraia. Urusi, ambayo rasmi ina hazina kubwa zaidi ya silaha za nyuklia, iliyorithiwa kutoka kwa USSR, na Iran wamepiga hatua kubwa kwa mawasiliano yao tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine mnamo 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *