
Katika msimamo unaokumbusha muhula wake wa kwanza, Donald Trump ameamua kupiga marufuku raia wa nchi 12 kuingia Marekani ili “kuilinda” nchi dhidi ya “magaidi wa kigeni,” na kuweka vikwazo kwa mataifa mengine saba. Uamuzi umetangazwa, alibainisha, baada ya shambulio la Colorado ambalo lililenga washiriki katika maandamano ya kuunga mkono mateka wa Israeli huko Gaza. Licha ya maelezo haya, marufuku haya hayatumiki kwa Misri, nchi anakotoka mtu anayeshutumiwa shambulio hilo.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Marufuku hiyo ambayo itaanza kutekelezwa Juni 9, inazihusu Afghanistani, Burma, Chad, Jamhuri ya Kongo, Equatorial Guinea, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Somalia, Sudani na Yemen, kulingana na Ikulu ya White House. Nchi nyingine saba zinakabiliwa na vikwazo: Burundi, Cuba, Laos, Sierra Leone, Togo, Turkmenistani, na Venezuela.
Serikali ya Marekani, ambayo inafuata sera kali sana ya kupinga uhamiaji, inahusisha uwepo wa nchi katika orodha hii na ukosefu wa tawala bora, tabia ya raia wa baadhi ya nchi kutaka kubaki nchini Marekani baada ya mudawa visa vyao kumalizika, na, kwa upande wa Iran, kwa kuunga mkono “ugaidi.”
Hata hivyo kuna watu ambao hawatahusika na hatua hiyowale ambao wana baadhi ya visa na kwa watu binafsi ambao safari yao kwenda Marekani “hutumikia maslahi ya taifa.” Wachezaji wa soka wanaoshiriki michuano ya Kombe la Dunia la 2026, ambayo itachezwa Marekani, Mexico, na Canada, pamoja na wanariadha katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028, hawataathiriwa na vikwazo.
Venezuela yaonya raia wake
Mnamo Juni 4, Venezuela ilionya raia wake kwamba kusafiri kwenda Marekani kunaleta “hatari kubwa.” “Kurejeshwa kwa marufuku hiyo hakutaifanya Marekani kuwa salama zaidi, lakini kutasababisha mateso kwa Wamarekani wengi, wakiwemo wale walio katika jamii ya Wamarekani wenye asili ya Iran, ambao wapendwa wao watanyimwa visa kiholela,” amelalamika Jamal Abdi, menyekiti wa National Iranian American Council..
Orodha hiyo haijumuishi Misri, nchi ambako anatoka mwanamume mwenye umri wa miaka 45 anayetuhumiwa kwa shambulio hilo, ambalo limesababisha Donald Trump kuhalalisha uamuzi wake. Katika video iliyorushwa kwenye mtandao wa wa X, rais wa Marekani amesema kwamba “shambulio la kigaidi la hivi majuzi huko Boulder, Colorado, magharibi mwa nchi hiyo, lilionyesha hatari kubwa inayoletwa Marekani na kuingia kwa raia wa kigeni ambao hawajachunguzwa ipasavyo. Hatuwataki,” almeongeza.
Siku ya Jumapili, Juni 1, huko Boulder, mwanamume mmoja aliwarushia mabomu ya petroli washiriki katika maandamano ya kila wiki ya kuwaunga mkono mateka wa Israeli wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza, na kuwajeruhi watu 12. Alipiga kelele akisema “Palestina Huru” wakati wa shambulio lake. Anatarajiwa kufikishwa mahakamani huko Colorado mnamo Juni 5 kuarifiwa rasmi mashtaka dhidi yake. Anashutumiwa, miongoni mwa mambo mengine, kwa “uhalifu wa chuki” na jaribio la kuua.
Mshambuliaji “aliingia Marekani kinyume cha sheria”
Utawala wa Marekani umesema kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa nchini Marekani “kinyume cha sheria,” kwa kuwa muda wake wa visa wa kitalii ulikuwa umekwisha. Hata hivyo, ilikiri kwamba aliomba hifadhi na aipata kibali cha kufanya kazi.
Donald Trump alilinganisha marufuku yake mpya ya kusafiri na “vizuizi madhubuti” alivyoweka kwa idadi ya nchi za Kiislamu wakati wa muhula wake wa kwanza (2017-2021), ambapo alidai kuwa iliizuia Marekani kukumbwa na mashambulio yaliyotokea huko Ulaya. “Hatutaruhusu yaliyotokea Ulaya kutokea Marekani,” amesema. “Hatuwezi kuwa na uhamiaji wa wazi kutoka nchi ambazo hatuwezi kudhibiti na kuchunguza kwa usalama na kwa uhakika,” rais wa Marekani amebainisha.
Wakati wa muhula wake wa kwanza, marufuku ya Waislamu ilisababisha machafuko katika viwanja vya ndege, na kesi ikaishia kwenye Mahakama ya Juu, ambayo iliidhinisha toleo lililorekebishwa. Mnamo Juni 4, Wademocrat walijibu mara moja, wakimshutumu Donald Trump kwa kuitenga zaidi Marekani kwenye jukwaa la kimataifa na kusaliti kanuni zilizotetewa na Mababa Waanzilishi.