
Baada ya mashambulizi katika miji ya Dioura, Boulikessi, na Timbuktu, kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM, lenye uhusiano na Al Qaeda) limedai kuhusika na shambulio huko Mamaribougou, nje kidogo ya mji wa Bamako, Jumatano, Juni 4. Pia kambi ya kijeshi ya Tessit huko Kaskazini katika eneo la Gao ilishambuliwa na wanajihadi siku ya Jumatano baada ya wanajeshi kuzidiwa kabisa na wanajihadi kutoka Islamic State katika Sahel.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Mali lilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika eneo la Kidal. Asubuhi ya Alhamisi, Juni 5, shambulio jipya limeripotiwa katika eneo la Sikasso, kusini mwa nchi.
“Kituo cha usalama” cha Mahou kwenye mpaka wa Burkina Faso, kimelengwa. Katika taarifa, jeshi lilionyeshalimebaini kwamba limeongeza idadi ya wanajeshi na magari ya kivita “ardhini na angani.” JNIM, kwa upande wake, imedai kuwa “imechukua udhibiti wa kambi.” Hakuna majeruhi wameripotiwa katika hatua hii.
Siku ya Jumatano, JNIM ilidai kuhusika na shambulio huko Mamaribougou, mji ulio katika wilaya ya Mandé, karibu na mji wa Bamako. Kundi la wanajihadi lilidai kuhusika na shambulio hilo, kwa kulenga “mkusanyiko wa jeshi la Mali na washirika wake wa Urusi” kutoka kwa kundi la Wagner kwa kutumia kifaa cha kulipuka kwenye “uwaja wa mazoezi”. Wakazi waliripoti kusikia kishindo kikubwa na kushuhudia ambulensi zikija na kuondoka.
Jeshi la Mali halijatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo. Hata hivyo, chanzo cha usalama cha Mali kimethibitisha kutokea kwa shambulio hilo, huku idadi ya wanajeshi wawili wa Mali wakiuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya. “Eneo la Mandé limevamiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja,” chanzo hicho kimeongeza.
Tessit, Eneo la mipaka mitatu
Upande wa kaskazini, katika eneo la mpakani la Mali, Niger na Burkina Faso, wanajihadi wapinzani wa Islamic State katika Sahel walichukua udhibiti kamili wa kambi ya kijeshi ya Tessit siku ya alasiri. Kambi hiyo huwa na makumi ya wanajeshi na wapiganaji wa Mali kutoka Gatia, kundi la wenyeji lenye silaha linaloshirikiana na vikosi vya Mali. Kundi la Wagner mara kwa mara hufanya operesheni katika eneo hilo, lakini kutoka mji wa karibu wa Ansongo na haliko Tessit, kulingana na vyanzo vya usalama vya ndani na raia viliowasiliana na RFI.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, wanajihadi walisababisha uharibifu mkubwa katika kambi hiyo na kuondoka na silaha nyingi na zana za kijeshi. Hakuna majeruhi ambao wangeweza kuthibitishwa. Jeshi la Mali lilithibitisha shambulio hilo na kuashiria kwamba lilikuwa limezindua “doria za anga” ambazo “zilipiga kwa nguvu” safu ya kigaidi katika “jaribio la kurudi nyuma,” bila kutoa takwimu zozote za majeruhi.
Mashambulio ya jeshi huko Kidal
Katika eneo la Kidal, vikosi vya Mali vilitekeleza mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Djanchéché/Yenchechi, takriban kilomita sitini magharibi mwa jiji la Kidal. “
Vyanzo vya kiraia pia vinaripoti shambulio huko Tadjemart, kusini mwa mji wa Aguelhoc, pia katika jimbo la Kidal. Vyanzo hivi vinadai kuwa raia walikuwa miongoni mwa wahanga wa mashambulizi haya, ikiwa ni pamoja na familia yenye wanawake na watoto.