Donald Trump kuhudhuria mkutano wa NATO nchini Uholanzi mwishoni mwa mwezi Juni

Rais wa Marekani Donald Trump atahudhuria mkutano wa kilele wa NATO, uliopangwa kufanyika Juni 24-25 huko Hague, Uholanzi, msemaji wake, Karoline Leavitt, ametangaza Jumanne, Juni 3. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangu arejee mamlakani, rais wa Marekani amekuwa akiwahimiza wanachama wa muungano wa ulinzi kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi yao ya kijeshi.

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte tayari amehakikisha kwamba nchini Uholanzi, nchi 32 wanachama wa Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini zitatangaza ongezeko “kabambe” la bajeti zao za ulinzi. 

Donald Trump anadai kwamba Canada na nchi za NATO za Ulaya zitoe angalau 5% ya pato lao la ndani (GDP) kwa ulinzi, wakati zingine zimetatizika kufikia kiwango kinachohitajika cha 2% hadi mwaka 2024.

Kwa miongo kadhaa, nchi za Ulaya kwa kiasi kikubwa zimekabidhi gharama ya usalama wao, iliyotolewa na Washington ndani ya mfumo wa NATO, kwa Marekani na kupunguza matumizi yao ya kijeshi.

Marekani, ambayo ilitumia karibu 3.3% ya Pato la Taifa katika ulinzi mwaka 2024, imekuwa ikikosoa udhaifu wa matumizi ya kijeshi ya Ulaya kwa miaka kadhaa. Donald Trump alisema mwezi Januari kwamba anaamini nchi wanachama wa NATO zinapaswa kutumia 5% ya Pato lao la Taifa kwa ulinzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *