Ushuhuda wa kuhuzunisha kutoka kwa watetezi wawili wa haki za kibinadamu walioteswa Tanzania

Shuhuda za kuhuzunisha kutoka Kenya. Mnamo Juni 2, jijini Nairobi, watetezi wawili wa haki za binadamu wa Kenya na Uganda, Boniface Mwangi na Agather Atuhaire, wameelezea mazingira ambamo walikamatwa na kuzuiliwa nchini Tanzania. Walikamatwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita, walikokuja kuhudhuria kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Baada ya kuzuiliwa kwa siku tatu bila mawasiliano, walifukuzwa  na kurejeshwa kila mmoja nchini mwake. Mnamo Juni 2, walielezea mazingira ya kuzuiliwa kwao.

Ni katika hoteli walikofikia, mapema jioni, ambapo Boniface Mwangi na Agather Atuhaire walikamatwa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Baada ya kupita idara ya Uhamiaji na kisha kituo cha polisi, walichukuliwa na maafisa wa usalama wa ndani. Usiku, mikono yao imefungwa na kufungwa macho, walipelekwa kwenye jengo lisilojulikana. Huko, walivuliwa nguo na kisha kutundikwa kichwa chini. “Hapo walianza kunipiga miguuni kwa nguvu huku wakinihoji, ‘unaitwa nani, unatoka wapi, nani amekutuma, kwa nini umekuja kuhatarisha usalama wa nchi yetu? Kisha kijana mmoja akaniwekea mafuta kwenye sehemu yangu ya siri ya nyuma na kuanza kuniingizia vitu, akaniomba niseme, ‘Asante Samia,’ hivyo nikamshukuru rais wa Tanzania,” anaeleza Boniface Mwangi.

Karibu naye, Agather Atuhaire aliteswa vibaya kama alivyoteswa mwenzake: “nilivuliwa nguo zote ni kabaki uchi, nilidhalilishwa, vipigo na hatimaye kubakwa. Wakati akiwa kizuizini kwa siku tatu, ubalozi wa Uganda haukuonyesha kujali hatima yake. Agather Atuhaire, anasema eneo lote la Afrika Mashariki linahusika. “Nilijua siku nitakayoteswa ingefika. Naishi na hofu hii Uganda, lakini sikujua ingeweza kutokea Tanzania, ambako sikufanya lolote kabisa, hata kuandamana. Viongozi wa Tanzania hawakuogopa hata kidogo kwa yale waliyotufanyia. Kwangu mimi, hiki ni kiwango cha kutokujali ambacho siwezi kufikiria. Sisi kama raia wa Afrika Mashariki, sisi weyewe ndo tunaweza kushughulikia kwanza matatizo yetu.”

Katika taarifa yake jana, mungano wa mashirika ya kiraia katika kanda hiyo umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhamasishwa dhidi ya dhulma na ghasia zinazoripotiwa katika nchi za katika Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *