
Wakati huu wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, raia wa Burundi ingawa wamechoka lakini wanajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa wabunge wa Juni 5 ambao umepoteza mvuto na kukosekana kwa washindani wa kweli.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Zikiwa zimesalia siku mbili, mrengo wa upinzani umelalamikia ukosefu wa mafuta,vitisho na kushambuliwa kwa wanaharakati na chama tawala cha CNDD FDD ,kama baadhi ya maswala ambayo yameathiri kampeni za mrengo huo.
Patrick Nkurunziza Rais wa muungano wa Burundi Bwa bose, amesema wiki tatu za kampeni zimekuwa ngumu kwa vyama vya upinzani, tofauti na upande wa chama tawala, ambacho kimeendeleza kampeni kubwa bila kupungukiwa na rasilimali.
Hata hivyo wananchi wanachojali kwa sasa ni gharama ya juu ya maisha, hali ambayo imewafanya kutochangamkia uchaguzi huo wa Alhamisi.
Wanadiplomasia wameelezea wasiwasi kuwa kwa hali ilivyo inaonekana matokeo ya uchaguzi huo tayari yamefahamika.
Waandishi wa habari ambao wametumwa kufuatilia uchaguzi huo, hawataruhusiwa kuripoti matokeo tofaut na yale yatakayotangazwa na CENI la sivyo watakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka mitano hadi kumi jela.