Aucho, Mukwala wachemsha Uganda

Aucho, Mukwala wachemsha Uganda

KIUNGO nyota wa Yanga, Khalid Aucho na mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala wamechemsha huko Uganda baada ya kushindwa kubeba tuzo  tuzo za mashabiki kwa wachezaji wanaocheza nje.

Tuzo hizo zilizofanyika Mei 30, chini ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Aucho na Mukwala waliangushwa Rodgers Mato, aliyeibuka mshindi.

Mato ambaye ni mshambuliaji anayeichezea klabu ya Vardar ya Marcedonia Kaskazini, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Katika kipengele hicho,  Aucho, Mukwala na Mato walikuwa wakichuana na Elio Capradossi (SC Cittadella-Italia) na Bevis Mugabi (Anorthosis Famagusta-Cyprus).

Mbali na Mato, wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka 2024 walitunukiwa tuzo hizo za FUFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *