Nyuklia: Tehran inadai ‘dhamana’ kutoka Marekani juu ya kuondolewa kwa vikwazo

Iran imeitaka Marekani leo Jumatatu, Juni 2, kutoa “dhamana” juu ya kuondolewa kwa vikwazo vinavyokandamiza uchumi wa nchi hiyo, kufuatia pendekezo la Marekani la uwezekano wa makubaliano ya nyuklia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tunataka hakikisho kwamba vikwazo vitaondolewa,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghai amesema. “Hadi sasa, upande wa Marekani haujataka kufafanua suala hili,” ameongeza wakati wa mkutano wa kila wiki mjini Tehran, kulingana na shirika la habari la AFP.

Iran ilififisha matumaini ya Marekani kuhusu uwezekano wa kufikiwa makubaliano, huku ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), likiishutumu Tehran kwa shughuli katika maeneo kadhaa ya nyuklia ambayo hayajatangazwa.

Mjumbe Maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati Steve Witkoff amewasilisha kwa Iran “pendekezo la kina na linalokubalika,” kulingana na Ikulu ya White House, lenye lengo la kuunganisha misimamo kuhusu kurutubisha nyuklia. Iran imesema haitaacha haki yake ya kurutubisha madini ya uranium iwapo itakubali makubaliano au la, huku Marekani ikisema kurutubisha madini ya uranium ni mstari mwekundu ambao Iran haipaswi kuuvuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *